Avengers katika sinema hivi karibuni

Post 16 of 32
Avengers katika sinema hivi karibuni

Katika kutizama kwangu filamu za marvel ,The avengers-watazamaji hatutaweza subiri mpaka mwisho wa filamu kushangiria kwani katikati ya action sequence katika onyesho la tatu la story, team nzima ya avengers,ikijumuisha Iron man, Hulk, Thor,  Captain america, Hawkeye, na Black Widow, wana assemble kwenye screen na kufanya mtazamaji kubaki na butwaa.Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani filamu hii livyo tengenezwa kwa umakini mkubwa na jinsi waigizaji wake wanavyo weza kusadifu uhusika wao na jinsi dialogue na script vilivyo tengenezwa kwa umakini pia.

Avenger ni muendelezo wa baadhi ya ya filamu za marvel universe. Filamu inaanza pale Loki (Tom hilddleston) anaporudi tena dunia na kuiba “the Tesseract” an alien source of pure energy, na kutishia kuteka dunia nzima kwa msaada wa jeshi lake la viumbe kutoka dunia nyingine liitwalo “the chitauri”.

Nick Fury (Samuel L. Jackson), kiongozi wa covert government outfit inayoitwa  S.H.I.E.L.D anaunda team ya super heroes iitwayo The Avengers (Robert Downey Jr,Chris Hemsworth, Chris Evans, Mark Ruffalo, Scarlett johnsson, Jeremy Renner)  kuzuia mipango ya Loki.

Badalaya kufocus sana kwenyemuhusika mmoja, mwandishi /director Joss Whedon ametengeneza The Avengers katika balance. Na kuhakikisha kila muhusika anapata at least action sequence moja,wahusika wote wanaonekana na kupata nafasi ya kuwa na sehemu zao kwenye filamu. Captain America anahangaika kuuelewa ulimwengu mpya aliojikuta, Thor anamaumivu ya kumpoteza kaka yake, Iron man anakiburi na hataki kukosolewa au Hulk na woga wa nguvu alizonazo.Hata black widow na Hawkeye ambao hawakupewa kipaumbele katika mionekano yao ya mwanzo wanapata nafasi ya kuonekana, hivyo tuna pata uelewa mzuri zaidi wa wahusika hawa kwa kutumia pia backstories.

Filamu nyingi za marvel zimekuwa na action kidogo ila The Avengers ina rekebisha ilo ikionekana kutumia falsafa ya “go big or go home” na action yake imepangiliwa na inakwenda na story pia Whedon anafanya cut kwenye filamu hii ili kutuonyesha kila kinachoendelea kwa heroes tofauti . The final battle kati ya superhero team na jesh la Loki ni better kuliko action zote kwenye filamu za marvel pamoja na uzidishe kwa kumi.

Whedon anajulikana kwa kutengeneza wahusika wenye akili,upeo na kukua ki hisia, na filamu hii inaendeleza umaarufu huo.filamu hii pia ina furahisha  kote kwenye dialogue na hata physical humor( ambapo Loki anapambana na Hulk). Japokuwa inaanza kama imepooza ila inakuja pamoja haraka pale mwandishi/director anapo fanikiwa kuelezea story na kuchanganya high-tension fight na action sequence.

This article was written by POPOTE

Menu