Umejipanga utaongea nini kwenye ukurasa wa kampuni yako katika mitandao ya kijamii?

Post 11 of 32
Umejipanga utaongea nini kwenye ukurasa wa kampuni yako katika mitandao ya kijamii?

Makampuni mengi yanarahisisha mtazamo wao kuhusiana na social media marketing. Wengi wanadhania jambo la muhimu ni kufungua tu kurasa kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Youtube au kua na blog. Bila kufikiria nini watakachokua wanaongelea kwenye kurasa hizo.

Ni muhimu kwa kampuni kujihusisha katika matangazo kupitia mitandao ya kijamii lakini jambo la muhimu zaidi ni kujua nini utakionge na jinsi kitakavokusaidia kupata wateja wa bidhaa au huduma zako.

Ili uweze kujua nini cha kuongea ni lazima kuandaa mkakati (social media strategy). Zifuatazo ni hatua za kutengeneza Mkakati (social media strategy); 1. Weka malengo na madhumuni(Set goals and objectives) 2. Tambua viashiria (Determine metrics) 3. Watambua watu unaowalenga 4. Tafuta mtandao wa kijamii ulio sahihi kwako (Discover the right platform) 4. Andaa vitendea kazi na tambua majukumu (Gather resources and determine roles) 5. Tengeneza maudhui/utakachoongea (create content).

Maudhui inayoweza kukupa mafanikio ni kama kutoa mfululizo wa makala/taarifa za fursa zilizopo kwenye sekta uliopo au jinsi gani watumiaji wa huduma mbali mbali wanaweza kunufaika zaidi katika sekta hio. Pia kutoa makala/taarifa zenye ubora zinazoelezea kiundani juu a bidhaa au huduma zako, zinaweza kuongeza hamasa ya watu kua karibu na kampuni yako zaidi na pia jamii itakuchukulia kama mtaalamu katika sekta hiyo.

Kuandika juu ya ulichokula asubuhi au foleni barabarani haitawanufaisha sana wafuasi wako, lakini na wewe pia hautanufaika.

Je una mkakati tayari……..? Unajua cha kuandika kwenye kurasa zako mtandaoni…..?

, , , , ,

This article was written by @odhiamboluis

Menu