Umuhimu wa tovuti kwa biashara yako

Post 5 of 32
Umuhimu wa tovuti kwa biashara yako

Ukitazama biashara nyingi za kati au ndogo zina kitu kimoja zinafanana, nyingi hazina tovuti au website zinazotoa maelezo ya kutosha juu ya huduma, bishaa au eneo zinakofanya kazi. Iwe ni hapa nyumbani Tanzania au kwenye nchi zinazoendelea pekee, bali hata kwenye nchi za ulimwengu wa kwanza, hali ipo hivo. Biashara nyingi huendeshwa na familia na nyingi hufanya kazi kimazoea.

Magdalena ni mmiliki wa saluni ya kike iliyopo katikati kabisa ya jiji la Dar es Salaam, anasema “Japo najua umuhimu wa kuwa na tovuti lakini ni gharama sana kuitengeneza na hata kuihudumia, nadhani nahitaji kuajiri mtu mwenye ujuzi wa mambo hayo, jsmbo ambalo siwezi kwa sasa”

Inawezekana kuwa ni kweli gharama ni kubwa, au wenye biashara hawajui umuhimu wa tovuti, au pengine hawajui kabisa kitu chochote kuhusiana na tovuti. Makala haya yatajaribu kueleza kwa uchache, umuhimu hasa wa tovuti/website kwa biashara yako, na kukupa mbinu za kuweza kupata tovuti kwa njia rahisi, bila kuhangaika kuajiri mtaalamu. Kabla hatujaendelea zaidi, hebu tujiulize. Je internet ni nini?

Intaneti ni nini?

Intaneti ni mtandao wa kompyuta zilizoenea duniani kote zote zikiwa zimeunganishwa moja kwa nyingine. Unapojiunga kwenye Intaneti unakuwa na ufikiaji wa World Wide Web, ambayo ni sawa na maktaba iliyojaa kurasa za maelezo. Kurasa hizi huwa na maelezo mbali mbali, na kwa pamoja huitwa tovuti/wavuti.

Tovuti ni nini?

Tovuti ni mkusanyiko wa kurasa zilizoandikwa kwa lugha mbalimbali za tarakilishi kama vile HTML, PHP, XHTML na kadhalika na ambazo kwa pamoja hujumuika katika kutoa habari au maelezo kuhusu jambo fulani. Jambo hili huweza kuwa ni taarifa za biashara yako. Hivyo basi, ukitengeneza tovuti ya biashara yako, ni kama kuweka taarifa za biashara yako katika maktaba ya dunia. Maktaba ambayo inaweza kufikiwa na mtu yoyote mahali popote, saa yoyote na hii ndio sababu ya msingi kabisa ya kutengeneza tovuti yako.

Umuhimu wa tovuti kwenye biashara yako.

Kwanza ni rahisi zaidi wateja kujua kuhusu biashara yako na huduma unazozitoa. Kutokana na maendeleo ya sayansi ya teknolojia, watu wengi ni watumiaji wa internet. Ni rahisi zaidi kwao kutafuta taarifa za biashara yako kupitia mtandao au “ku Google” kama inavyojulikana kwa jina la mitaani. Je wateja wako wanapo “GOOGLE” na kuikosa biashara yako mtandaoni wanachukua hatua gani? Jibu lipo wazi, watahamia kwa mshindani wako kibiashara, jambo ambalo naamini hulitaki, ndio hata mimi au yoyote hawezi kufurahia mpinzani wake kumwibia wateja. Hii ni sababu mojawapo ya kuwa na tovuti, ili wateja wanaopenda “ku google” wakupate kirahisi zaidi.

Pili tovuti inaongeza thamani ya biashara yako. Tovuti yako inaweza kubadili mtazamo wa mteja wako, na kuona kuwa ni biashara kubwa zaidi ya ilivyo. Hii si tu itakuongezea imani kwa wateja, pia inaweza kuongeza wateja wengi zaidi na imani yao kwako. Ni rahisi mtu kufanya biashara na kampuni anayoijua vyema, je ni wapi atapata taarifa zako? Je atasoma kwenye mabango mitaani taarifa za fedha za kampuni za mwaka uliopita? Au ataona kwenye tangazo la televisheni juu ya mashine mpya mnazotumia kutengeneza bidhaa? Jibu ni hapana. Ni sehemu moja tu unayoweza kuweka taarifa zako zote, nayo ni tovuti.

Tengeneza tovuti yako leo

Baada ya kuona sababu chache kati ya nyingi za biashara yako kuhitaji tovuti, hebu basi tutazame, je unawezaje kupata tovuti?

Njia ya haraka, inayojulikana na wengi ni kuwa ukitaka tovuti lazima uajiri kampuni au walau “WEB DESIGNER” ili akufanyie kazi hiyo. Pia utahitaji kulipia “hosting” na “domain name”.

Makampuni haya huwa na gharama kubwa, kwa wastani utahitaji zaidi ya dola za kimarekani 500 na kuendelea ili uweze kupata tovuti, hii ni gharama kubwa sana kwa wafanyabiashara wa wadogo na wa kati. Ni wazi kuwa, zaidi ya gharama pia utahitaji muda mrefu kupata tovuti yako, mara nyingi huwa mwezi mmoja au zaidi. Baada ya kupata tovuti, tatizo jingine huzaliwa, ujuzi. Kuhudumia tovuti kunahitaji umakini na utaalamu fulani, makampuni haya hutoa mafunzo kwa wateja wao jinsi ya kufanya, jambo ambalo sio bay isipokuwa ni gumu sana kwa baadhi ya watu.

Hadi hapo utaona ugumu wa kutengeneza tovuti, pengine hii ni sababu ya kwa nini wamiliki wengi wa biashara za kati na ndogondogo wanaacha kutengeneza tovuti za biashara yao. Lakini je vipi kama nitakueleza njia mbadala, njia rahisi zaidi ya kuweza kutengeneza tovuti ya biashara yako, bila kuajiri kampuni kubwa, bila kuhofia gharama na zaidi ya yote kufanya kila kitu mwenyewe?

WEB2MOBI ni suluhisho la kudumu la kuwawezesha wafanyabiashara wa kati na wadogo kujitengenezea tovuti zao za biashara au za binafsi kupitia simu zao za mikononi. Ndio umenisikia vyema, kupitia simu yako ya mkononi.

Hii ni huduma mpya nchini tanzania, inayokuwezesha kutengeneza tovuti, au kubadili tovuti uliyonayo kuwa katika mfumo wa tovuti inayoonekana vyema kwenye simu za mkononi, vyote hivi katika muda mfupi kabisa.

Huhitaji kujua HTML au kugha nyingine tarakaishi, unachagua kurasa zilizotengenezwa tayari na kuhariri kufuata na unavyopenda wewe. Pia unaweza kuweka sauti, video na picha mbalimbali za biashara yako. Tovuti hii inakuwezesha kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na biashara yako, ina fomu mbalimbali ili kukusanya taarifa za wateja, na kama utataka unaweza kuweka eneo ilipo biashara yako ili kuwawezesha wateja kukupata kirahisi. Hii ni kidijitali zaidi.

Tafadhari, bonyeza hapa WEB2MOBI kulike page yetu ya Facebook ili uweze kupata maelezo zaidi ya jinsi ya kujiunga na huduma hii bora na rahisi zaidi nchini Tanzania. WEB2MOBI Simu yako, Tovuti yako. Kidijitali zaidi.

 

This article was written by Gervas

1 comment:

KouNovember 22, 2013 at 6:43 amReply

When you think about it, that’s got to be the right answre.

Menu